Kamusi ya Magonjwa ya binadamu

Profesa Evariste Ntakirutimana
Chuo Kikuu cha Rwanda
Butare

Dictionnaire


concept n° Mag-0001

[SW]

Définition : vidonda vya kinywani.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0002

[SW]

Définition : kosefu au upungufu wa sukari mwilini.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0003

[SW]

Définition : hali ya mwili ya kutendana kupita kiasi dhidi ya dutu fulani punde dutu hiyo inapoingia mwilini.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0004

[SW]

Définition : ugonjwa unaoenezwa kwa vinywaji visivyo safi na salama vyenye bakteria jamii ya amiba; bakteria hawa husababisha mgonjwa kuhara damu, vidonda vya tumbo na kukosa hamu ya kula.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0005

[SW]

Définition : usahaulifu wa matukio ya nyuma.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0006

[SW]

Définition : upungufu wa chembe nyekundu za damu ama hemoglobini.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0007

[SW]

Définition : ukosefu wa usingizi au shida ya kupata usingizi.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0008

[SW]

Définition : kiwasho cha kooni.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0009

[SW]

Définition : ukosefu wa mkojo kutokana na kutokuwepo ama kupungua kwa unywesaji katika figo.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0010

[SW]

Définition : kiwasho cha kidoletumbo au kibole.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0011

[SW]

Définition : ukosefu wa unyeo.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0012

[SW]

Définition : hali ya kutohisi baridi.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0013

[SW]

Définition : ukosefu wa hamu ya kula.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0014

[SW]

Définition : ugonjwa maarufu kwa watoto ambao husababishwa na mvurugano katika seli za ubongo, husababisha homa na huonyesha dalili kama za kifafa.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0015

[SW]

Définition : hali ya kutuna kwa mishipa ya vena katika eneo la chini la rektamu kutokana na mlundikano wa damu.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0016

[SW]

Définition : ugonjwa unaotokana na upungufu wa vitamini B1 mwilini.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0017

[SW]

Définition : ubronkitisi ya kudumu.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0018

[SW]

Définition : kivimbe chenye majimaji katika ngozi.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0019

[SW]

Définition : hali ya akili kuparanganyika.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0020

[SW]

Définition : kiwasho cha bronkasi.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0021

[SW]

Définition : uvimbe mfano wa jipu kinenani.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0022

[SW]

Définition : kuvimba kwa jicho lote kutokana na kuziba tangu kuzaliwa kwa vijia vya kupita kioevu cha jicho; husababisha glaukoma ya kuzaliwa.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0023

[SW]

Définition : uvimbe mdogo wenye majimaji katika ngozi.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0024

[SW]

Définition : uvimbe au basa ya kanyagio hasa katika kifundocha kidole gumba.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0025

[SW]

Définition : ugonjwa unaosababisha mishipa ya uume kuvimba na kuufanya kutanuka kuliko kawaida; huweza kuenea sehemu yote ya kinena.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0026

[SW]

Définition : maumivu ya mkono.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0027

[SW]

Définition : vipele vitokeavyo mwilini hususan usoni, hutokea mara nyingi kwa vijana wanaobarehe na kuvunja ungo.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0028

[SW]

Définition : uumwaji wa tumbo.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0029

[SW]

Définition : hali ya kupoteza uwezo wa kiubongo kwa kiasi kikubwa.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0030

[SW]

Définition : homa kali ya nchi za joto inayoenezwa na mbu wa Aedesi.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0031

[SW]

Définition : hali ya kutotamka maneno vizuri kutokana na lesheni katika mfumo mkuu wa neva.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0032

[SW]

Définition : hali ya kutoweza kutoa sauti vizuri.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0033

[SW]

Définition : kujisikia vibaya.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0034

[SW]

Définition : hali ya kushindwa kutamka maneno ipasavyo kutokana na matatizo ya akili.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0035

[SW]

Définition : maumivu wakati wa kukojoa.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0036

[SW]

Définition : kuathirika kwa utoaji wa nyongo kutoka katika kibofu cha nyongo kutokana na misuli ya sfinkita ya odi kuwa katika hali ya mikazo.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0037

[SW]

Définition : hali ya kushindwa kutamka maneno sawasawa kutokana na athari katika ogani ya sauti au neva za ogani hizo.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0038

[SW]

Définition : hali ya kutoweza kusoma vizuri kutokana na lesheni katika mfumo mkuu wa neva.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0039

[SW]

Définition : ugumu wa kubainisha mawazo kwa njia ya kuyasema.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0040

[SW]

Définition : maumivu wakati wa hedhi.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0041

[SW]

Définition : hali ya kukisia vibaya umbali wakati wa tendomota kutokana na lesheni katika mfumo mkuu wa neva.Définition : kuathirika kwa uwezo wa kukadiria uzito wa vitu vilivyoekwa katika mikono yote miwili kutokana na lesheni ya ubongo wa serebelamu.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0042

[SW]

Définition : hali ya kutoweza kufanya ishara kama kawaida kutokana na lesheni ya ubongo.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0043

[SW]

Définition : hali ya kupumua kwa shida.Définition : hali ya kupungukiwa na pumzi.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0044

[SW]

Définition : hali ya kutoova vizuri.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0045

[SW]

Définition : hali ya kutoona vizuri.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0046

[SW]

Définition : hali ya kuzaliwa ambapo mtu huundika vibaya kwa mifupa.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0047

[SW]

Définition : uundwaji tishu usiokuwa wa kawaida.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0048

[SW]

Définition : hali ya kuwa na maumivu wakati wa kufanya chochote kile.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0049

[SW]

Définition : hali ya kutoweza kutenda kilichokusudiwa.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0050

[SW]

Définition : kuvurugika kwa tumbo kutokana na kuathirika kwa umeng’enyaji.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0051

[SW]

Définition : hali ya kutokufunga vyema kwa mfuo neva wa awali (kiinitete).

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0052

[SW]

Définition : matatizo katika toni ya tishu.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0053

[SW]

Définition : kutoka kwa ogani katika sehemu yake ya kawaida.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0054

[SW]

Définition : ugonjwa wa koo unaoambukiza ambao husababisha kupumua kwa shida aghalabu kwa watoto wadogo.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0055

[SW]

Définition : maradhi yaambukizwayo kwa njia ya zinaa ambayo vipele huota kwenye sehemu za uzazi na katika eneo linalozizunguka na mkunduni, husababishwa na kundi la virusi lijulikanalo kama human papilloma virus (HPV).

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0056

[SW]

Définition : maradhi ya virus aina ya EVD ambavyo husambazwa kutoka kwa wanyama pori kwenda kwa binadamu na kisha binadamu huanza kuambukizana wao kwa wao kwa njia ya kugusana.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0057

[SW]

Définition : hali ya kuvuja damu katika ubongo.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0058

[SW]

Définition : hali ya kutoweza kuzuia haja kubwa.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0059

[SW]

Définition : hali ya kutokwa damu puani.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0060

[SW]

Définition : uvimbe wowote wa ufizi.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0061

[SW]

Définition : tatizo la kuwapo kwa tundu au matundu karibu na njia ya haja kubwa ambapo huwa na mfereji unaojitokeza katika njia ya haja kubwa kwa ndani na hupitisha choo kikubwa bila ya mgomjwa kujitambua au kufahamu na tatizo hili huwakumba wanawake na hata wanaume.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0062

[SW]

Définition : jipu la foliko.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0063

[SW]

Définition : uvimbe wenye kioevu kizito.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0064

[SW]

Définition : kufa kwa sehemu ya mwili kutokana na kukosa mtiririko wa damu.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0065

[SW]

Définition : maumivu ya tumbo.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0066

[SW]

Définition : ugonjwa unaoshambulia neva za macho na kuyapelekea ulemavu baada ya muda na wakati mwingine kusababisha upofu.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0067

[SW]

Définition : ugonjwa wa viungo vya uzazi na mkojo unaosababishwa na bakteria Neisseria gonorrea.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0068

[SW]

Définition : hali ya kutokwa na damu ukeni inayowapata kila mwezi wasichana waliofikia umri wa kubarehe.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0069

[SW]

Définition : ugonjwa wa kutokwa damu ambapo damu hutoka kwa wingi kufuatia jeraha hata dogo; hutokea kwa watu wa kiume tu iwapo hurithiwa kwa kupitia kwa akina mama.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0070

[SW]

Définition : kutoka kwa damu.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0071

[SW]

Définition : kujichomoza kwa sehemu ya, au kwa kiungo chote cha ndani ya kaviti ya mwili.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0072

[SW]

Définition : kiwasho cha tishu parenkima ya ini.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0073

[SW]

Définition : ugonjwa wa malengelenge katika ngozi au membreni ute unaosababishwa na virusi vya hepesi.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0074

[SW]

Définition : ugonjwa wa kuzidi kwa kiwango cha sukari mwilini.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0075

[SW]

Définition : usingizi wa kupita kiasi.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0076

[SW]

Définition : kupanda kwa halijoto ya mwili.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0077

[SW]

Définition : upungufu wa chumvi ya kalsi mwilini.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0078

[SW]

Définition : halijoto ya mwili iliyo chini kuliko kiwango cha kawaida.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0079

[SW]

Définition : hali ya kupanda kwa joto mwilini kupita kiasi.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0080

[SW]

Définition : tatizo linalosababishwa na baridi kuathiri mwili kwa kupenya katikati ya mifupa.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0081

[SW]

Définition : maumivu makali ya viungo na kichwa ambayo hurudia kila baada ya siku tatu na hufuatiwa na ahueni ya muda mrefu; husababishwa na virusi na huenezwa na mbu aina ya Aedes.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0082

[SW]

Définition : augonjwa ambao husababishwa na virusi ambavyo hushambulia chembechembe za ini na hivyo ini kushindwa kufanya kazi zake ipasavyo, mara nyingi ini huvimba na pengine hupasuka.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0083

[SW]

Définition : ugonjwa wenye kuanishwa na homa kali, uchovu na mwili kuwa manjano.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0084

[SW]

Définition : aina ya homa inayoupata uti wa mgongo, itokanayo na vimelea jamii ya fungus, ambayo huweza kushambulia ubongo pia na husambazwa kwa njia ya hewa.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0085

[SW]

Définition : ugonjwa wa ngozi wa kuzaliwa ambapo ngozi huwa kavu na yenye magambamagamba.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0086

[SW]

Définition : ugonjwa wa ngozi kuwa na upele wenye usaha.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0087

[SW]

Définition : mafua makali ya virusi vya influenza.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0088

[SW]

Définition : alama, mkwaruzo anaoupata mtu baada ya kuumizwa na kitu chenye ncha.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0089

[SW]

Définition : jeraha la ngozi linalotokana na baridi kali.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0090

[SW]

Définition : jeraha litokanalo na kuunguzwa na kiowevu cha moto.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0091

[SW]

Définition : mkusanyiko wa usaha katika tishu kutokana na uambukizo wa vimelea.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0092

[SW]

Définition : hali ya kupanuka kwa moyo.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0093

[SW]

Définition : kiwasho cha moyo wote.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0094

[SW]

Définition : kujipinda kwa mgongo.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0095

[SW]

Définition : kujipinda kwa mgongo kuelekea mbele na upandeni.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0096

[SW]

Définition : ugonjwa utokanao na kuzaliana kwa seli kusiko kwa kawaida katika kiungo cha mwili na kukiharibu na kisha kusambaa sehemu nyingine za mwili.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0097

[SW]

Définition : ugonjwa ambao hupelekea kuharibika kwa kumbukumbu na kuvuruga mfumo mzima wa ufanyaji kazi wa ubongo.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0098

[SW]

Définition : maradhi yanayosababishwa na bakteria wajulikanao kama Treponema pallidum na dalili zake ni vipele katika sehemu za uzazi huanza kujitokeza muda mfupi baada ya maambukizi ambayo baadae hupotea yenyewe.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0099

[SW]

Définition : ukungu wa lenzi la jicho au wa kapsuli yake.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0100

[SW]

Définition : ugonjwa ambao hupelekea mchafuko wa tumbo na mara nyingi matokeo yake ni kutapika.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0101

[SW]

Définition : ugonjwa unaosababishwa na minyoo ijulikanayo kama schistosomes ambayo huathiri utumbo na kibofu na dalili zake ni kuhara na kukojoa damu.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0102

[SW]

Définition : maumivu kwenye mapafu yanayosababishwa na baridi kali.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0103

[SW]

Définition : uvimbe wa mwili unaozidi kiasi kutokana na kupigwa na kitu au mtu.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0104

[SW]

Définition : hali ya kuvimba kwa ncha za kidole, mkono au mguu kufuatia magonjwa wa kudumu mwilini.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0105

[SW]

Définition : kidonda kinachotokana na kulalia upande mmoja wa mwili kwa muda mrefu.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0106

[SW]

Définition : kugonjwa wa kikohozi cha muda mrefu unaosababishwa na bakteria ambapo mwathirika hukohoa kwa kutoa sauti kubwa.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0107

[SW]

Définition : ugonjwa wa kurithi ambao husababisha ubongo kupoteza mawasiliano na mtu kuzimiazimia ghafla.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0108

[SW]

Définition : ugonjwa ambao husababishwa na bakteria mbalimbali ambazo hujulikana kama mycobacterium tuberculosis na huathiri mapafu na sehemu zingine za mwili ambao dalili zake ni kikohozi sugu, kukohoa damu, homa, kutokwa jasho jingi usiku na kukonda.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0109

[SW]

Définition : shambulio la ghafla la kupooza kutokana na kuvuja damu au kuziba kwa mshipa wa damu katika ubongo.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0110

[SW]

Définition : hali ya kutoa kwa ghafla hewa nyingi mapafuni pamoja na sauti kubwa ya kufunguka glotisi.Définition : ugonjwa wa kifaduro.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0111

[SW]

Définition : ugonjwa wa ghafla wa kuumwa upande mmoja wa kichwa unaoambatana na kichefuchefu, kutapika na matatizo ya kuona.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0112

[SW]

Définition : maradhi ya kuharisha na kutapika ambayo husababishwa na bakteria iitwayo vibrio-cholerae.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0113

[SW]

Définition : maumivu ya misuli ya mikono yatokanayo na kuandika kwa muda mrefu.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0114

[SW]

Définition : muwako anaouhisi mtu sehemu ya ndani ya kifua ambao husabishwa na tindikali kupanda toka tumboni kuelea kooni.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0115

[SW]

Définition : hali ya mwili kuwa na sukari nyingi kupita kiasi au upungufu wake, husababishwa na udhaifu wa kongosho kushindwa kutoa insulin ya kutosha kuyeyusha sukari iliyomo kwenye chakula.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0116

[SW]

Définition : hali ya kuhisi mwili ama mazingira kuzunguka na kumfanya mtu kukosa nguvu na kuzirai.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0117

[SW]

Définition : ugonjwa wa zinaa unaosababishwa na bakteria wajulikanao kama Chlamydia trachomatis ambao hawaonyeshi dalili za wazi kwa karibu 75% ya wanawake na 50% ya wanaume, hivyo maambukizi mengi hushindwa kufahamika mapema; husababisha usaha kutoka kwenye uke au uume na hupelekea kuwashwa wakati wa hedhi.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0118

[SW]

Définition : utapikaji wa nyongo.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0119

[SW]

Définition : unyesaji wa nyongo.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0120

[SW]

Définition : kuziba kwa utiririkaji wa nyongo.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0121

[SW]

Définition : kiwasho cha uke.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0122

[SW]

Définition : kansa yenye koloidi.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0123

[SW]

Définition : kushuka chini kuliko kawaida kwa utumbo mpana.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0124

[SW]

Définition : kutoka kwa damu ukeni.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0125

[SW]

Définition : upotezaji wa fahamu.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0126

[SW]

Définition : uvimbe wa ngozi katika maeneo ya unyeo au ya sehemu za uzazi.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0127

[SW]

Définition : uvimbe mgumu wa ngozi.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0128

[SW]

Définition : jeraha litokanalo na kupigwa na dutu butu ambapo ngozi huwa haichaniki.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0129

[SW]

Définition : kujipindapinda kwa ogani.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0130

[SW]

Définition : mkusanyiko wa kinyesi kigumu katika utumbo.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0131

[SW]

Définition : kukonda kwa mwili kunakotokea taratibu.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0132

[SW]

Définition : hali ya kukosekana kwa haja kubwa au kuipata kwa shida.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0133

[SW]

Définition : ugonjwa wa kuhara damu au kwenda haja kubwa ambayo imechanganyika na damu.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0134

[SW]

Définition : hali ya kwenda haja laini mara kwa mara kuliko kawaida.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0135

[SW]

Définition : kupungukiwa na sauti ama kuwa na sauti inayokwamakwama.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0136

[SW]

Définition : kuharibika kwa jino na kuanza kutoboka ama kutoa vipandevipande.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0137

[SW]

Définition : maradhi ambayo husababishwa na virusi ambavyo hupenya kwa njia ya chakula na dalili zake ni shingo kukakamaa na homa kali.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0138

[SW]

Définition : hali ya ngozi kupungua unene na kuwa na makunyanzi kutokana hususan na uzee.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0139

[SW]

Définition : kupishana kidogo kwa mifupa inayokutana.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0140

[SW]

Définition : kuhisi ubaridi mwingi.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0141

[SW]

Définition : hali ya kuwa na maumivu ya kichwani.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0142

[SW]

Définition : upoteaji wa fahamu wa muda kutokana na kupungua kwa mtiririko wa damu ubongoni.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0143

[SW]

Définition : ugonjwa wa mfumo wa neva ambao unahusiana na uambukizo wa homa ya rumatiki.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0144

[SW]

Définition : hali ya kusinyaa ghafla kwa ukuta utenganishao kifua na tumbo ambayo husababisha kufunga ghafla kwa koo la hewa na kutoa mlio kwi.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0145

[SW]

Définition : ugonjwa wa ngozi unaosababishwa na vimelea vya kuvu.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0146

[SW]

Définition : tatizo la maambukizi kwenye kucha ambalo huwapata wazee kuanzia miaka sabini na kuendelea.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0147

[SW]

Définition : maambukizi ya bakteria katika njia ya mkojo ambayo huweza kuenezwa kutoka mtu mmoja kwenda mtu mwingine kwa njia ya kujamiiana, huweza kuenea kwenda juu mpaka kwenye kibofu cha mkojo na hata kwenye figo.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0148

[SW]

Définition : ugonjwa wa sikio ambao husababishwa na bakteria wapenyao katika ngoma ya sikio na kuiharibu na wakati mwingine kutunga usaha.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0149

[SW]

Définition : ugonjwa wa ngozi ambapo rangi ya mwili hupotea na kuacha mabakamabaka meupe.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0150

[SW]

Définition : athari mbaya za sehemu ama ya ogani ya mwili.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0151

[SW]

Définition : maradhi ya kuambukiza ambayo husababishwa na virusi ambavyo huenea wakati mgonjwa anapokohoa au kupiga chafya karibu na watu wengine.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0152

[SW]

Définition : ugonjwa ambao hushambulia mfumo wa mapafu katika mwili wa binadamu na ambao huenezwa kwa kula vyakula vya ndege, kama kuku, bata, kanga na kadhalika.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0153

[SW]

Définition : maradhi ya kulalalala ambayo husababishwa na wadudu jamii ya mbung’o pale wananapomng’ata binadamu na kumwambukiza bakteria, hukaa ubongoni na siyo rahisi kupona bila matibabu thabiti.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0154

[SW]

Définition : ugonjwa ambao huenezwa na mbu jike aina ya anofelesi.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0155

[SW]

Définition : aina ya ukurutu inayoweza kuwatokea wanawake na wanaume ambao huenezwa kwa njia ya kujamiiana.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0156

[SW]

Définition : upoteaji fahamu wa muda mfupi unaoambatana na kutoona kutokana na upungufu wa mtiririko wa damu ubongoni.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0157

[SW]

Définition : maradhi ambayo huambukizwa kwa kugusana kati ya mgonjwa na asiye mgonjwa na ambapo kuvu hushambulia eneo la kichwa peke yake.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0158

[SW]

Définition : hali inayoathiri umbile, utendaji kazi ya mwili wote ama sehemu zake.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0159

[SW]

Définition : maumivu ya titi.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0160

[SW]

Définition : utolewaji tumboni kwa ghafla kwa vilivyomezwa kupitia kinywani.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0161

[SW]

Définition : ugonjwa unaosababisha uvimbe wa matezi mwili mzima.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0162

[SW]

Définition : hali ya kuhisi uchungu.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0163

[SW]

Définition : ugonjwa ambao aghalabu huwapata watu kutokana na umri mkubwa na kupelekea mtu kutembea akiwa ameshika mkongojo.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0164

[SW]

Définition : chembechembe ndogondogo ambazo hupatikana katika mfumo wa mkojo na kusababisha maumivu makali yakiambatana na homa.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0165

[SW]

Définition : ugonjwa wa mabaka katika ngozi unaotokana na kuvu.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0166

[SW]

Définition : mwachano wa tishu utokanao na matumizi ya nguvu za kuzidi kiasi.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0167

[SW]

Définition : homa ya uti wa mgongo.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0168

[SW]

Définition : msitari utokanao na pindo la ngozi mwilini.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0169

[SW]

Définition : ugonjwa ambapo sehemu ya mwisho ya utumbo mkubwa mkunduni (rectum) hujitokeza nje kutokana na kudhoofika au kuachana kwa kapilari na kuta za utumbo mkubwa.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0170

[SW]

Définition : hitilafu ya kutoona vitu vya mbali.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0171

[SW]

Définition : kujikunja kwa misuli kunakoambatana na maumivu.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0172

[SW]

Définition : mlipuko wa vipele mwilini ambavyo husababisha mwili kuwasha na mtu kujikuna ambavyo mara nyingi huhusishwa na dalili za maambukizi ya virusi vya ukimwi.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0173

[SW]

Définition : hali ya kutoa sauti kama filimbi inayotoka katika njia za kupumua ambazo zimepungua upenyo wake.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0174

[SW]

Définition : hali ya kusimana kwa ridhimu ya moyo.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0175

[SW]

Définition : hiparemia ya ogani au sehemu ya ogani.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0176

[SW]

Définition : hali itokanayo na kuwa na mambo mengi kichwani na kufanya mtu awaze kama haiwezekani yakafanyika yote kwa ukamilifu.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0177

[SW]

Définition : utokaji wa mfupa kutoka katika nafasi yake ya kawaida.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0178

[SW]

Définition : ugonjwa unaoathiri sehemu ya ubongo ambayo hushughulika na mijongeo ya mwili ambayo dalili zake huonekana zaidi wakati wa uzee.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0179

[SW]

Définition : hali ambayo mfupa hukatika kutokana na ajali fulani.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0180

[SW]

Définition : ugonjwa mkali wa kuambukiza unaofanana na surua na ambao hutokeza upele mwingi wenye majimaji na usaha.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0181

[SW]

Définition : maumivu ya figo.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0182

[SW]

Définition : ugonjwa wa mapafu.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0183

[SW]

Définition : kidonda cha shavu na kinywa au cha vulva na uke ambacho huenea kwa haraka na kutokea kwa baadhi ya watoto wenye utapiamlo mkali.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0184

[SW]

Définition : kiwasho cha mapafu ambapo yanakuwa na konsolidesheni.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0185

[SW]

Définition : ukondefu wa mwili unaotokana hususan na upungufu wa lishe.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0186

[SW]

Définition : kiwasho cha sikio.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0187

[SW]

Définition : maambukizi makali yasababishwayo na bakteria ambayo hupelekea kusinyaa kwa misuli ya taya na shingo na baadaye kuenea mwili mzima, sehemu zote zinaonekana kukaza na huambatana na homa kali na mgonjwa hupata taabu kupumua.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0188

[SW]

Définition : hali inayosababisha kuzuiliwa kwa hewa kwenye mapafu na kufanya iwe vigumu kupumua.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0189

[SW]

Définition : utokaji wa damu puani.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0190

[SW]

Définition : ugonjwa wa kuvimba tezi kwenye shingo.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0191

[SW]

Définition : kiwasho cha kifundo inayoambatana na homa.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0192

[SW]

Définition : kansa ya uterasi.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0193

[SW]

Définition : kansa ya matiti.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0194

[SW]

Définition : kansa ya tezi dume au kansa ya kibofu.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0195

[SW]

Définition : ugonjwa wa ukurutu kama vile hepesi.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0196

[SW]

Définition : esheni ya awali ya kaswende ambayo huanza kama kivimbe kigumu ambacho baada ya siku chache kidonda hujitokeza katikati yake ilihali pembezoni mwake hubakia kuwa pagumu.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0197

[SW]

Définition : kidonda katika sehemu za uzazi kinachotokana na uambukizo wa kujamiiana wa bakteri Hemofilasi dukreyi.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0198

[SW]

Définition : ugonjwa ambao msukumo wa damu kwenye mishipa huwa mkubwa kuliko kawaida na kusababisha moyo kufanya kazi kupita kiasi na kuweza kusababisha madhara kama vile mzio na kiharusi.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0199

[SW]

Définition : maradhi ya neva ambapo ngozi ya mwili huwa na malengelenge na maumivu makali katika mtandao wa neva athirika.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0200

[SW]

Définition : hali ya kupunguka kwa kupita kiasi kwa shinikizo la damu.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0201

[SW]

Définition : kiwasho cha sinasi.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0202

[SW]

Définition : uharibifu wa tishu parenkima za ogani unaoambatana na kuongezeka kwa wingi wa tishu ya utembwe.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0203

[SW]

Définition : kiwasho cha kibofu cha mkojo.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0204

[SW]

Définition : ugonjwa wa kutoka damu katika ufizi kutokana na upungufu wa vitamini C.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0205

[SW]

Définition : ugonjwa wa kudumu wa akili ambao aghalabu huanza katika miaka ya mwanzoni ya utu uzima.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0206

[SW]

Définition : kupindika upande kwa mgongo.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0207

[SW]

Définition : ugonjwa wa kizunguzungu ambacho huambatana na kuona alama nyeusi machoni.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0208

[SW]

Définition : kuongezeka kwa ukubwa wa bandama.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0209

[SW]

Définition : ugonjwa wa kuhara wa muda mrefu unaoambatana na kutoa choo cha mafuta, vidonda vya kinywani kukonda na anemia.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0210

[SW]

Définition : maradhi ambayo husababishwa na virusi jamii ya morbillivirus paramyxovirus na huenezwa kwa njia ya hewa au upumuaji, dalili zake ni mgonjwa kutokwa mafua mepesi, homa kali, kikohozi, macho kuwa mekundu na kutokwa vipele vidogovidogo usoni, masikioni na kisha mwili mzima.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0211

[SW]

Définition : maradhi ambayo husababishwa na bakteria aina ya salmonella na dalili zake ni mgonjwa kuumwa kichwa mara kwa mara, homa kali na ikichelewa kutibiwa hutoboa utumbo mpana na kuweza kusababisha kifo.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0212

[SW]

Définition : hitilafu katika utengenezwaji wa cheni za peptidiza hemoglobini.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0213

[SW]

Définition : mlipuko mkubwa wa ugonjwa hususan wa dunia nzima.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0214

[SW]

Définition : ugonjwa unaosababishwa na bakteria na huweza kuambukizwa kwa njia ya hewa na kugusana, huenezwa sana na panya.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0215

[SW]

Définition : ugonjwa wa kitropiki ambao husababishwa na vimelea vinavyoshambulia matezi na kusababisha kiungo aghalabu miguu kuvimba kupita kiasi.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0216

[SW]

Définition : maradhi ya virus yenye kuambukiza sana haswa nyakati za utotoni na dalili zake za awali ni homa ndogo, mwili kuwa dhaifu kwa ghafla au kutokujisikia vizuri na kupoteza hamu ya kula; vipele vinavyowasha hutokeza mgongoni halafu hutapakaa usoni na kisha sehemu zingine za mwili.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0217

[SW]

Définition : ugonjwa wa kuambukiza kwa njia ya vitone ambao husababishwa na bakteria wa tiibi.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0218

[SW]

Définition : maradhi ambayo husababishwa na maambukizi ya protozoa anayofahamika kisayansi kama Trichomonasivaginalis na maradhi haya hupelekea muwasho katika uke na kuhara kwa wanawake na kwa wanaume husababisha maumivu katika njia ya mkojo.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0219

[SW]

Définition : ugonjwa wa kuziba kiasi fulani au kuziba kabisa kwa atari koronari na moyo kutokana na kibonge cha damu.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0220

[SW]

Définition : ukosefu wa nyege.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0221

[SW]

Définition : hali ya kupungukiwa nguvu.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0222

[SW]

Définition : hali ambayo mwili hukosa nguvu ambayo mara nyingi huwa ni dalili ya homa au maambukizi ya ugonjwa fulani.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0223

[SW]

Définition : hali ya kukonda kusiko kwa kawaida.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0224

[SW]

Définition : hali ya kutokwa na mkojo bila ya kukusudiwa.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0225

[SW]

Définition : ugonjwa utokanao na figo kushindwa kufanya kazi vizuri kwa muda wa miezi, miaka na kuja kugundulika figo zikiwa zimeshaathirika sana.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0226

[SW]

Définition : ugonjwa wa kurithi ambao husababisha mtu kupoteza kumbukumbu kwa muda mfupi.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0227

[SW]

Définition : hali ya kutokuwa na uwezo wa kuzaa.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0228

[SW]

Définition : hali ya mwanamme kutoweza kufanya mapenzi.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0229

[SW]

Définition : hali ya kukojoa kitandani wakati mtu akiwa usingizini ambayo huanza wakati wa utoto na kuendelea mpaka ukubwani kwa baadhi ya watu.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0230

[SW]

Définition : upungufu wa kinga mwilini ambao husababishwa na virusi vishambuliavyo viini kinga vya mwili na kisha kudhoofisha mfumo wa kinga dhidi ya magonjwa ambukizi na nyemelezi.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0231

[SW]

Définition : ukosefu wa uwezo wa kusikia ambayo huweza kuwa ya muda au ya kudumu.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0232

[SW]

Définition : ugonjwa unaosababishwa na bakteria microbacterium leprae ambaye huenezwa kwa njia ya kugusana na mwathirika kwa muda mrefu na dalili zake ni vidonda vya ngozi na kuathirika mfumo wa neva katika baadhi ya viungo vya mwili wa binadamu.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0233

[SW]

Définition : muwasho wa ngozi ambao husababisha ngozi kuwa nyekundu na kuota vipele vidogovidogo vyenye majimaji ndani.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0234

[SW]

Définition : ukosefu wa kiungo fulani cha mwili au hali ya kiungo fulani kutofanya kazi yake ipasavyo.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0235

[SW]

Définition : hali ya kurithi ambayo mtu hawezi kurefuka zaidi ya urefu wa kawaida.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0236

[SW]

Définition : ugonjwa ambao humfanya mtu kuwa na mwili mkubwa na uzito usio wa kawaida.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0237

[SW]

Définition : ugonjwa wa kurithi ambao mara nyingi huwapata wanaume na husababisha nywele kunyonyoka.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0238

[SW]

Définition : hali ya kutoweza kuona kutokana na matatizo ya muda au ya kudumu.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0239

[SW]

Définition : utokaji magamba mwilini.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0240

[SW]

Définition : ukosefu/upungufu wa maji mwilini.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0241

[SW]

Définition : ugonjwa wa macho au ngozi unaosababishwa na aina fulani ya minyoo midogo ya filaria ambayo huenezwa na nzi wadogo weusi aina ya simulium.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0242

[SW]

Définition : ugonjwa ambao huathiri akili na kumfanya mtu afanye mambo yasiyoeleweka.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0243

[SW]

Définition : utoa damu kupitia kinywani.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0244

[SW]

Définition : gonjwa unaotokana na utendaji kazi wa kupita kiasi wa glandi thiroidi.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0245

[SW]

Définition : ukosefu au upungufu wa melanini mwilini.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0246

[SW]

Définition : hali ya kuvimba kwa tezi za kooni na kusababisha homa kali.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0247

[SW]

Définition : michubuko inayotokea kwenye kuta za ndani za tumbo ikitokana na tindikali inayozalishwa na mfumo wa mmengenyo wa chakula, ambayo mara nyingi hutokana na kutokula chakula kwa muda wake au msongo wa mawazo.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0248

[SW]

Définition : hali ya kutokuwa na akili timamu.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0249

[SW]

Définition : ugonjwa wa ngozi ambapo ngozi hukauka na kuwa ngumu na baadye kutoa magamba madogomadogo.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0250

[SW]

Définition : ugonjwa unaosababishwa na virusi ambavyo husambazwa na aina ya mbu wanaong’ata wakati wa mchana.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0251

[SW]

Définition : ugonjwa wa kuvimba tumbo aghlabu kwa unaosababishwa na jicho la husuda.

[EN]

[FR]


concept n° Mag-0252

[SW]

Définition : magonjwa yenye asili ya wanyama ambayo pia huweza kuenezwa kwa binadamu.

[EN]

[FR]

Index

Index Swahili

English Index

Index français